MITAZAMO NA MAONI YA WATANZANIA JUU YA RUSHWA 2017 - TWAWEZA
Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli imezindua mikakati mipya ya kupambana na rushwa. Mikakati hii ni pamoja na kuanzishwa kwa mahakama mahsusi kwa ajili ya kushughulikia kesi za rushwa. Mkakati mkubwa kabisa umekuwa ni kuchukua hatua za papo kwa hapo kupambana na tuhuma za rushwa na vitendo vingine vya ubadhirifu. Wafanyakazi wa mamlaka ya bandari na mapato walifutwa au kusimamishwa kazi pale ushahidi ulipobainisha kwamba kulikuwa na ukwepaji wa kodi bandarini.
view reportdownload