MAONI YA WATANZANIA KUHUSU KUKWAMA KWA MCHAKATO WA MAREKEBISHO YA KATIBA 2017 - TWAWEZA
Mchakato wa kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulianza baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Vyama viwili vikuu vya upinzani nchini, CHADEMA na CUF ndivyo vilivyoanzisha vugu vugu ya kudai katiba mpya. Umuhimu wa katiba mpya ndio ulikuwa msingi wa kampeni za uchaguzi za vyama hivyo. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliitikia wito huo kwa kuanzisha mchakato wa marekebisho ya Katiba. Hata hivyo mchakato huo ulisimama mwaka 2015, kupisha uchaguzi mkuu wa 2015, na haujaendelea tena tangu kipindi hicho.
view reportdownload